Bieber, Selena sasa mambo shwari

Image result for Bieber, Selena
Hatimaye nyota wa muziki wa Pop nchini Marekani, Justin Bieber na aliyekuwa mpenzi wake, Selena Gomez, wamemaliza tofauti zao.

Wawili hao walikuwa kwenye uhusiano kuanzia mwaka 2011 na wakaja kuachana 2014, baada ya kuachana walikuwa hawaongei kwa kipindi chote hicho, lakini sasa wameamua kumaliza tofauti zao.

Selena, mwenye umri wa miaka 25, hivi karibuni alikuwa anasumbuliwa na tatizo la figo na kufanyiwa upasuaji, hivyo mrembo huyo akaamua kumpigia magoti Bieber, mwenye umri wa mioaka 23, na kuomba wayamalize.

Kwa mujibu wa TMZ, wawili hao wameweza kumaliza tofauti zao, lakini hawajaweka wazi kwamba wataendelea kuwa wapenzi kama ilivyo zamani.

No comments

Theme images by lobaaaato. Powered by Blogger.