Chris brown ‘amzimia’ Jennifer LopezNyota wa muziki wa RnB nchini Marekani, Christopher Brown ‘Chris Brown’, amefunguka kwa mara ya kwanza na kusema kuwa anampenda sana Jennifer Lopez.

Msanii huyo, ambaye kwa sasa hajamuanika mpenzi wake tangu aachane na mwanamitindo Karrueche Tran, lakini sasa amedai anampenda na kumhitaji Jennifer Lopez.

Amedai bila kujali umri wa Jennifer, lakini anatamani kuja kuishi na mrembo huyo mwenye umri wa miaka 48, huku Chris akiwa na umri wa miaka 28.

“Ninaamini ujumbe wangu ataupata Jennifer Lopez kuwa ninampenda na ninahitaji kuwa na yeye, bila kujali umri alionao, hata kama angekuwa na miaka 70, lakini bado ningeonesha hisia zangu kwake,” alisema Chris.

No comments

Theme images by lobaaaato. Powered by Blogger.