Diamond awapiga chini Ali Kiba, Darassa tuzo za AfrimmaMsanii wa kimataifa kutoka Tanzania Diamond Platnumz ajinyakulia tuzo ya Afrimma katika kipengeke cha  Msanii bora wa kiume  Afrika Masharika.

Diamond Platnumz amenyakua tuzo hiyo na kuwapiga chini wasanii wawili kutoka Tanzania Darassa pamoja na Ali Kiba ambao nao walikua katika kinyang’anyiro hicho ambacho Diamond ameibuka kinara.

Tuzo za Afrimma mwaka huu zimetolewa mjini Dallas, Texas nchini Marekani huku zikipambwa na wasanii mbalimbali ambao walipanda jukwaani kwa ajiri ya kufanya ‘show.’akiwemo Diamond na Rayvanny kutoka Tanzania.

Ushindi huu alioupata Diamond Platnumz ni ushindi wa Taifa zima na unatoa hamasa kwa wasanii wengine kuweka jitihada zaidi ili kuongeza wasanii wengi zaidi wanao tuwakilisha kimataifa.

No comments

Theme images by lobaaaato. Powered by Blogger.