Dogo Janja kumuoa Irene Uwoya… ni filamu au kikiNa: Omary Ramsey

Ukiachana na harusi ya mchekeshaji Lucas Mhaville ‘Joti’ aliyofunga mwishoni mwa wiki iliyopita, tetesi za msanii wa Bongo Fleva, AbdulAzizi Chande ‘Dogo Janja’ kudaiwa kufunga ndoa na Irene Uwoya, ndio imekuwa habari ya mjini kwa sasa.

Maswali mengi yamebaki kwa mashabiki wa muziki na Bongo Movie wakishindwa kuelewa kama kuna ukweli wowote juu ya hilo, huku msanii huyo wa Bongo Fleva, Dogo Janja, kuendelea na msimamo wake wa kutotaka kuzungumzia uhusiano wake.

Ingawa picha mbalimbali zilizozagaa zinamwonyesha Irene pekee akiwa kwenye vazi la harusi bila ya Dogo Janja, lakini mrembo huyo aliandika kwenye mtandao wake wa Instagram: “Nimeolewa na mwanamume wa ndoto zangu, bado nalia machozi ya furaha, nakupenda (akimtag Dogo Janja), nafurahi uwepo wako kuwa sehemu ya maisha yangu.”Tangu kuibuka kwa tetesi kwamba wawili hao wana uhusiano, Dogo Janja amekuwa akikanusha uhusiano huo, lakini Irene naye hakuwahi kuthibitisha kabisa kuwa ni mpenzi wa msanii huyo.

Mara kwa mara Dogo Janja amekuwa akisema kwamba amekuwa akimkubali Irene tangu akiwa mdogo na mara nyingine hata kusema maneno makali kwamba, msanii huyo wa Bongo Movie ni kama mama yake kutokana na kumzidi kiumri.

“Irene ni mfano wangu wa kuigwa tangu nikiwa mdogo nimekua namfuatilia sana, naheshimu kuwa ni mke wa mtu na nitaendelea kumkubali na siwezi kusikiliza maneno ya watu ambayo naona ni jambo la kawaida kadiri siku zinavyokwenda,” anasema Dogo Janja.

Irene Uwoya ambaye ni mama wa mtoto mmoja, alifunga ndoa na mwanasoka Hamad Ndikumana mwaka 2012 na kufanikiwa kuzaa naye mtoto mmoja aitwaye Krish, huku wawili hao wakitengana baada ya kushindwa kuelewana na kila mmoja kuendelea na maisha yake.

Swali linalobaki kwa Watanzania ni kweli wawili hao wamefunga ndoa, wanatafuta kiki au ni filamu? Kama ni ndoa kwanini bibi harusi ndio anaonekana peke yake bila ya bwana harusi?

No comments

Theme images by lobaaaato. Powered by Blogger.