Hatimaye Mkubwa Fella athibitisha ujio mpya wa Maromboso


Mkubwa Fella ambaye alikuwa anawasimamia Yamoto Band amethibisha ujio wa aliyekuwa member wa Band hiyo Mamborosso baada ya wasanii wa kundi hilo kuanza kufanya kazi as a solo project.

Kauli ya Fella inakuja wakati kukiwa na mshawasha kuwa huenda msanii huyo akatambulisha ngoma yake ya kwanza akiwa chini ya label ya WCB kama iliyodokezwa hivi karibuni na Diamond Platnumz.

Kwenye mahojiano yake na Bongo5 Jumatatu hii, Fella amesema “Kikubwa wameshakua na unaona Aslay, Beka na inshallah mwezi huu mtamsikia Marombosso japokuwa mmemsikia kwenye ngoma ya Zilipendwa kaonekana nini alikifanya lakini kikubwa kingine kuna ngoma yake mpya inakuja mwezi huu, mtaona kinachofanyika,”

October 3 mwaka huu ambapo Marombosso alikuwa akisheherekea siku yake ya kuzaliwa, Diamond katika kumtumia salamu za pongezi kupitia mtandao wa Instagram alidokeza pia ujio wa msanii huyo.

“Kheri ya siku ya kuzaliwa Marombosso maneno kamwe hayatoweza kutosha kuelezea ni kiasi gani mie mshabiki wako. Heshima na Busara zako hunifunza mengi, nasubiria kwa hamu siku ya utambulisho wako rasmi kama Msanii na Mwanafamilia wa WCB Wasafi vile vile ulimwengu kusikia kipaji kingine kizuri kutoka Tanzania,” aliandika Diamond.

Credit: Peter Akaro (@Bongo5)

No comments

Theme images by lobaaaato. Powered by Blogger.