Madee, Nandy kunani! msikie hapa Madee..Msanii Madee ammwagia sifa msanii wa kike Nandy anaefanya vizuri sasa na wimbo wake wa Wasikudanganye kwa kusema kuwa ni miongoni mwa wasanii watatu wa kike ambao wanafanya vizuri kwa sasa.

Madee amesema kuwa hakuwahi kufanya wimbo na msanii wa kike na wakatengeneza wimbo mkubwa kama ilivyo kwa Nandy na wimbo wao wa Sema ambao unazidi kufanya vizuri katika chati mbalimbali za Radio na Runinga.

‘’Nilipo amua kufanya kazi na msanii wa kike nilimuangalia Nandy kwakuwa ni miongoni mwa wasanii watatu ambao wanafanya vizuri kwa sasa na siwezi kusema anashika namba ngapi kati ya hao wasanii wa kike watatu lakini kikubwa nayeye ni miongoni mwao’’ amesema madee.

Hata hivyo, made ameongeza kuwa hakupata tabu kufanya kazi na Nandy na wala hakumsumbua kwani alipokea ombi lake la kumshirikisha na wakafanya kazi kwa muda muafaka.

No comments

Theme images by lobaaaato. Powered by Blogger.