R. Kelly kazi anayo unaambiwaMambo si mazuri kwa upande wa mwanamuziki R. Kelly, ambapo mwanamke mwingine ameibuka na kusema aliwahi kumtesa.

Hii si mara ya kwanza kwa R. Kelly kukutwa na kashfa hiyo kwani tayari kuna orodha ndefu ya wanawake waliowahi kumshutumu.

Mwanamke huyo aitwaye Kitti Jones, alisema aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na msanii huyo zaidi ya miaka miwili iliyopita. Alisema alikutana naye kwa mara ya kwanza mwaka 2011 katika ‘party’ moja mjini Dallas na kuanzia hapo walianza kutumiana meseji kabla ya kuzama kwenye penzi zito.

Jones aliongeza kuwa kwa kipindi chote cha ukaribu wao, alikuwa akidundwa na R. Kelly na staa huyo alikuwa na wanawake wengi.

Mwanadada huyo ambaye ni DJ wa moja ya redio mjini Dalas, alisema mwaka mmoja baadaye alilazimika kuacha kazi na kuhamia kwenye mjengo wa R. Kelly uliopo Chicago.

Mtihani wa kwanza aliokutana nao Jones ni msanii huyo kumtaka asiwe anavaa nguo nzuri, kwa madai ‘atawatega’ wanaume watakaokuwa wakifika nyumbani hapo.

Haikuishia hapo, Jones aliongeza kuwa mwaka 2013 alidhalilishwa zaidi na R. Kelly baada ya mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 50, kumtaka afanye mapenzi na wanawake wenzake.

“Asilimia 99 ya kipindi chote hicho, sikuwa nataka kufanya na hata nilikuwa nikimwambia kuwa sipendi,” alisema Jones. Baada ya miezi sita, ndipo Jones alipoamua kuondoka kumkimbia R. Kelly, akimdanganya kuwa alikuwa anamfuata mtoto wake.

Miezi miwili baadaye, wakakutana na Jones alisema staa huyo alimtolea lugha chafu.

No comments

Theme images by lobaaaato. Powered by Blogger.