Adele akataa shoo ya Bilioni 2Na: Omary Ramsey

Nyota aliyetamba na wimbo wa ‘Hello’ Adele Adkins, amekataa kufanya shoo mbili zenye thamani ya pauni milioni 1, ambazo ni zaidi ya bilioni 2 za Kitanzania.

Mrembo huyo mwenye umri wa miaka 29, mapema wiki hii alipelekewa mkataba na meneja wake ili ausaini kwa ajili ya kwenda Bara la Asia kufanya matamasha mawili ya muziki, lakini alidai hawezi kwa kuwa anapambana kuiweka sawa bustani yake.

Mapema mwaka jana msanii huyo alitajwa kuwa miongoni mwa wasanii wenye fedha nyingi kwa upande wa wanawake, huku akitajwa kuwa na jumla ya pauni milioni 52.5, zaidi ya bilioni 153.

“Nilimpelekea Adele mkataba wa kufanya matamasha mawili ya muziki barani Asia ukiwa na thamani ya pauni milioni 1, lakini baada ya kuusoma alidai hayupo tayari kwa kuwa anaweka sawa bustani inayozunguka nyumba yake,” alisema meneja wa msanii huyo.

No comments

Theme images by lobaaaato. Powered by Blogger.