Barakah The Prince atupa shutuma nzito , kisa?

Baada ya kufungua account mpya ya YouTube na kupotea tena, msanii Barakah The Prince amedai kuwa wanaofanya mchezo huo ni Seven Mosha ambaye ni meneja RockStar4000 pamoja na mfanyakazi wa Mx Carter ambaye hakutaka kumtaja jina.

Barakah na Seven
Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Sometimes’ ameiambia E-Newz ya EATV kuwa watu hao wawili ndio anawashuku kufanya hivyo kwani wao ndio walikuwa na password za account zote mbili.

“Nilijaribu kutengeneza channel mpya ya YouTube achana na ile mwanzo iliyokuwa na matatizo na watu wa Rockstar4000 walikuwa wanaing’ang’ania. Kwa hiyo baada ya ku-upload video kuna jamaa moja hivi mfanyakazi ya Mx Carter akaniomba password zangu za YouTube kwa maana kuna kitu walikuwa wanataka kunisaidia baada ya hapo tukio likawa linajirudia ni lilelile” amesema Barakah.

“Kwa hiyo inavyooneka hapa hapa kati ya watu wa Mx Carter na Seven wanaofanya huo mchezo moja kwa moja nawalenga wao kwa sababu hamna mtu yeyote alikuwa na access zangu za YouTube za mwanzo mpaka za pili tofauti na wao” amesisitiza.

Pia ameongeza kuwa suala hiyo tayari limeshafunguliwa kesi mahakamani. Barakah aliwahi kuwa chini ya usimamizi wa RockStar4000 na baadae kujitoa.

No comments

Theme images by lobaaaato. Powered by Blogger.