Bifu la Kanye, Jay Z chanzo ‘demu’ tu

398eea8900000578-3865720-shade_he_said_jay_z_did_not_visit_him_after_his_wife_kim_kardash-a-51_1477279632188


Na: Omary Ramsey

Mtandao wa Gossip Cop ambao ni maarufu kwa habari za mastaa, umefichua kilicho sababisha uadui uliopo sasa kati ya Kanye West na rafiki yake wa zamani, Jay Z.

Gossip Cop umesema Kanye anaamini kuwa Jay Z na mkewe, Beyonce, hawamheshimu mama watoto wake, Kim Kardashian.

“Hilo linamchanganya sana Kanye, kuona Beyonce anamchukulia poa Kim na kumwona si anayefaa kuwa rafiki yao. “Kama Beyonce na Jay Z, hawatakuwa tayari kumfanya Kim kuwa rafiki yao, basi hata yeye atawapotezea.

Vyanzo hivyo vilitolea mfano tukio la wiki iliyopita la Beyonce na Kardashian kuonekana kuwa karibu katika party ya ndoa ya staa wa tenisi, Serena Williams.

No comments

Theme images by lobaaaato. Powered by Blogger.