Blac Chyna anasa penzi la Playboi Carti

Image result for blac chyna playboi carti


Baada ya mwanamitindo maarufu nchini Marekani, Blac Chyna, kuachana na baba wa mtoto wake, Rob Kardashian, mrembo huyo sasa anaonekana kunaswa na penzi la rapa, Jordan Carter ‘Playboi Carti’, mwenye umri wa miaka 21.

Blac mwenye umri wa miaka 29, awali alikuwa anatoka na Tyga na kufanikiwa kupata naye mtoto kabla ya kudondokea kwa kaka wa Kim Kardashian, Rob na yeye kupata naye mtoto mmoja, lakini wawili hao wakaachana mapema mwaka huu ikiwa ni mwezi mmoja tangu wafanikiwe kupata mtoto.

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, uhusiano wa Blac na Playboi Carti ulianza tangu mrembo huyo bado yupo na Rob, lakini ulikuwa wa siri sana, hivyo baada ya kuachana kwao sasa wameamua kuuweka wazi kupitia kwenye mitandao ya kijamii.

Wiki iliyopita wawili hao walionekana wakiwa wamevaa nguo ambazo zinafanana wanakula chakula pamoja kabla ya baadaye kuonekana wakiwa ufukweni wakipata upepo.

No comments

Theme images by lobaaaato. Powered by Blogger.