CHRIS BROWN KUCHANGIA WAHANGA WA PUERTO RICO KWA NAMNA YA KIPEKEE

Chris Brown kuipiga bei picha ya heshima aliyomchora nguli wa Uchoraji, Andy Warhol.. kwa ajili ya kuchangia wahanga wa maafa ya kimbunga Maria kilichokimbuka kisiwa cha Puerto Rico.

Mwaka 2015 Breezy ambaye jina lake la usanii wa uchoraji anaitwa "Konfuzed" alishirikiana na mchoraji Karen Bystedt kuichora picha hiyo (Triple Andy Discount) ambayo kwa sasa wameipeleka sokoni kwenye mtandao wa eBay na inauzwa kwa mtu yeyote kwa dola za kimarekani Laki 5.
(Sawa na Tsh. 1,126,950,000/=)
-
Sehemu ya mauzo ya picha hiyo yataenda kusaidia wahanga wa kimbunga Maria 'Hurricane Maria', Puerto Rico.

No comments

Theme images by lobaaaato. Powered by Blogger.