CHUKI ZILITAWALA HUKUMU YA MEEK MILL

kiwa ni siku mbili tu zimepita tangu rapa mkali Meek Mill apigwe nyundo mbili (ahukumiwe miaka miwili) kwa kuvunja masharti ya muda wa chini ya Uangalizi (Probation) kwenye kesi yake ya kukamatwa na dawa za kulevya na kukutwa na silaha za moto ya mwaka 2008.

Mengi yaliibuka, mastaa wengi wamezungumza akiwemo Jay-Z, T.I, DJ Khaled, Rick Ross na wengine. Kikubwa hasa ni uonevu na ukiukwaji wa haki uliofanywa na jaji wa kesi hiyo.

Mwanasheria wa Meek Mill, Tacopina amefunguka Exclusive! Chuki binafsi na visasi vya jaji dhidi ya mteja wake na kisa kilipoanzia.

Akizungumza kwa njia ya simu na Billboard, Tacopina amesema, Jaji huyo, Bi. Genece Brinkley, alianza kumtaka Meek Mill afanye kuurudia wimbo wa kundi la Boyz II Men, "On Bended Knee" na ndani ya wimbo amalize kwa kumpa Shout out jaji huyo, yaani kumtaja jina... lakini Meek Mill alikataa.

Pili, ni pale jaji huyo (Genece Brinkley) alipomtaka rapa Meek Mill aachane na lebo ya Roc Nation na asimamiwe na mtu binafsi ambaye ni rafiki wa Jaji huyo. Meek Mill aligoma pia kufanya hivyo.

Kwa mambo hayo na mengine mengi, Jaji Genece alizalisha chuki binafsi dhidi ya Meek Mill na kupelekea kumhukumu miaka miwili jela.

Tayari Wakili Tacopina amepanga kukata rufaa.

No comments

Theme images by lobaaaato. Powered by Blogger.