Diamond kuachiwa Disemba hii A Boy From Tandale?

A Boy From Tandale inatoka Disemba 1 ya mwaka huu? Basi unaweza kukaa mkao wa kula kwa ajili ya kuisubiri albamu hiyo kutoka kwa Diamond Platnumz.


Japo msanii huyo kutoka WCB ameonekana kufanya siri kwenye hilo, lakini Dj na mtangazaji wa The Beat1036 FM, Ellie Prohan ameonekana kupenyezewa taarifa hizo na Diamond mwenyewe.


Kupitia mtandao wa Instagram, mrembo huyo ameweka picha akiwa na msanii huyo wakati alipotembelea katika kituo hicho cha radio na kuandika ujumbe unaosomeka, “When the Persian Power Met The POWER HOUSE @diamondplatnumz  #blessed #hallelujah @thebeat1036fm BIGGGGGG BANGER DROPPING 1st Dec #ABoyFromTandale #Hero !!! ”
Taarifa hizo zinaweza zikawa na ukweli ndani yake kwa kuwa hit maker huyo wa Hallelujah aliwahi kuahidi kuachia albamu yake ndani ya mwaka huu na itawakutanisha wasanii wakubwa duniani.

No comments

Theme images by lobaaaato. Powered by Blogger.