Droo ya Kombe la Dunia 2018 kufanyika Urusi

Baada ya mataifa 32 kufanikiwa kufuzu fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika mwakani nchini Urusi, droo ya kupanga makundi ya timu hizo itafanyika kesho Ijumaa mjini Moscow. 

Lionel Messi, the Kremlin and Thomas Muller

Kuelekea zoezi hilo baadhi ya Timu ambazo zimepangwa chungu kimoja ni chungu cha kwanza ambacho kina timu mwenyeji Urusi, Ujerumani, Brazil, Ureno, Ajentina, Ubelgiji, Poland na Ufaransa.
  • Mambo muhimu kuhusu nchi ambazo tayari zimefuzu Kombe la Dunia 2018
  • Taifa la watu 335,000 lafuzu Kombe la Dunia
Afrika inawakilishwa na Misri, Nigeria, Morocco, Tunisia na Senegal.
Na kuelekea fainali hizo FIFA wamesema mpaka sasa kuna maombi milioni 3.5 ya tiketi na walioomba wengi wao ni wenyeji Urusi.

Kombe la Dunia

Vyungu vimepangwa vipi?

Vyungu Kombe la Dunia
Chungu 1  Chungu 2 Chungu 3  Chungu 4
Urusi (wenyeji)   Uhispania (8)           Denmark (19)  Serbia (38)
Ujerumani (1) Peru (10) Iceland (21) Nigeria (41)
Brazil (2) Uswizi (11) Costa Rica (22) Australia (43)
Ureno (3) England (12) Sweden (25) Japan (44)
Argentina (4) Colombia (13) Tunisia (28) Morocco (48)
Ubelgiji (5) Mexico (16) Misri (30) Panama (49)
Poland (6) Uruguay (17) Senegal (32) Korea Kusini (62)
Ufaransa (7) Croatia (18) Iran (34) Saudi Arabia (63)

No comments

Theme images by lobaaaato. Powered by Blogger.