Enock Bella Nilitoa nafasi kwa Akina Aslay sasa ni wakati wangu

Msanii wa muziki Bongo, Enock Bella amesema ukimya wake katika game ulisababishwa na kutaka kutoa nafasi kwa wasanii wenzake waliokuwa pamoja Yamoto Band kusikika.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Sauda’ ameiambia 5Selekt ya EATV kuwa wangetoa ngoma wasanii wote wa Yamoto Band wangewachanganya mashabiki hivyo kupeana nafasi kungeepusha hilo.

“Kwanza nilikuwa natoa nafasi, unajua baada ya Aslay kuja akafuatia Beka, kisha Maromboso akaja kuonekana WCB kwa hiyo ilikuwa ngumu kama tusingeachiana nafasi ilikuwa tunawachanganya hata mashabiki lakini hii kuachia nafasi kidogo hata imesaidia kila mtu kutengeneza fan base yake” amesema Bella.

“Na mimi ndio maana nikaacha nafasi ili nitengeneze fan base yangu ili ninapokuja niwe na watu wangu na niwe na uwezo wa kufanya kazi mwenyewe” ameongeza.
Sauda ni ngoma ya kwanza kwa Bella kutoa tangu wasanii wa Yamoto Band kuanza kufanya kazi kama solo artist wakati Aslay akiwa ametoa ngoma zaidi ya 10, Beka ngoma mbili na Maromboso hajatoa ya kwake zaidi ya kusikika katika ngoma ya Diamond/WCB ‘Zilipendwa’.

No comments

Theme images by lobaaaato. Powered by Blogger.