GAVANA AINGILIA HUKUMU YA MEEK MILL

Kufuatia rapa #MeekMill kuhukumiwa kifungo cha miaka Miwili jela, imeripotiwa kuwa Gavana wa mji wa Pennsylvania Bwana Tom Wolfe, amesaini hati maalum ya Ombi (Petition) kwa lengo la Mahakama kutazama upya hukumu hiyo ambayo inadaiwa kutolewa kwa Uonevu na Ubaguzi.

Ombi hilo (petition) ambalo limelenga kuiomba Mamlaka husika kutazama upya hukumu hiyo, limeandikwa hivi,
"Meek Mill amekuwa sauti yenye nguvu kwa jamii yetu hasa vijana. Ametoa mchango mkubwa kwa jamii na miradi mbali mbali, akijitolea muda pamoja na pesa zake."
-

Ombi hilo maalumu kwa mamlaka husika (petition), limewekwa mtandaoni likihitaji kila aliyeguswa na hukumu hiyo iliyotolewa na Jaji Genece Brinkley, kuunga mkono kwa kusaini.

Mpaka sasa, watu Elfu 30 wamesaini huku ikilenga kufikia watu Elfu 35.

Credit @Info_HD


No comments

Theme images by lobaaaato. Powered by Blogger.