GRAMMY KUMPATIA JAY-Z HESHIMA HII KUBWA!

https://www.bet.com/topics/j/jay-z/_jcr_content/image.custom0x0.dimg/__1400807923247/2011-topic-music-jay-z-1.jpg
Nguli wa muziki wa Hip Hop duniani, JAY-Z, atatunukiwa Tuzo ya heshima ya Grammy (Salute to the Industry Icons Award) kwa mchango wake kama Nguli katika kukuza kiwanda cha muziki.

Jay ambaye ni mshindi mara 21 wa Tuzo za Grammy, atapatiwa Tuzo hiyo January 21, 2018 katika usiku wa sherehe za kabla ya kufanyika tukio kubwa la Ugawaji wa Tuzo za Grammy, (Pre-Grammy Gala) kwenye ukumbi wa Sheraton New York Times Square.Image result for Jay z

Kama ilivyowahi kutolewa kwa watu wengine kama Antonio "L.A" Reid, David Geffen na Debra L. Lee.. #JAYZ naye anaungana nao si tu kwa muziki wake bali mchango wake wa kutumikia kama Rais wa lebo kubwa ya Def Jam, umiliki wa mtandao wa Tidal, pia kuanzisha Tamasha kubwa la Philladephia's MADE IN AMERICA.

No comments

Theme images by lobaaaato. Powered by Blogger.