Harmonize kutumbuiza tuzo za Afrima
Staa wa muziki wa Bongo Fleva, Rajab Kahali ‘Harmonize’, leo anatarajia kudondosha bonge la burudani katika ufunguzi wa tamasha la siku tatu lenye lengo la kukuza muziki na tamaduni za Afrika litakaloambatana na utolewaji wa tuzo za All Africa Music (Afrima 2017) jijini Lagos, Nigeria.

Harmonize ni miongoni mwa mastaa wa muziki 95 watakaotumbuiza katika tamasha hilo ambalo linazinduliwa leo na kufuatiwa na burudani ya muziki katika Kijiji cha Afrima Music, ambapo kesho kutakuwa na sherehe ya wasanii wote waliotajwa kuwania tuzo hizo huku tuzo zikitolewa Jumapili.

Kutoka Tanzania wasanii ambao wanawania tuzo hizo mwaka huu ni pamoja na Ali Kiba na Diamond Platnumz kwenye kipengele cha Msanii Bora wa Kiume Afrika Mashariki na Nandy, Vanessa Mdee, Lady Jay Dee na Feza Kessy katika kipengele cha Msanii Bora wa Kike Afrika Mashariki.

Wasanii wengine ni Msafiri Zawose anayewania tuzo ya Msanii Bora wa Muziki wa Asili pamoja na Darassa kupitia wimbo wake wa Muziki anawania tuzo ya Msanii Bora Anayependwa na Mashabiki.

No comments

Theme images by lobaaaato. Powered by Blogger.