HUKUMU YA MEEK MILL: JAJI AZIDI KUKALIA KAA LA MOTO!Jaji aliyemuhukumu rapa Meek Mill kwenda Jela Miaka Miwili, amezidi kukalia kaa la moto baada ya maovu yake kuanza kubainika.

Kwa mujibu wa taarifa ya TMZ, imebainika kuwa Jaji Genece Brinkley alienda kinyume cha Sheria kwa kumruhusu Meek Mill akutane/ajihusishe na mtu mwenye rekodi ya makosa ya Jinai.

Hii ni baada ya kumtaka #MeekMill aachane na lebo ya ROC NATION na kazi zake zisimamiwe na jamaa anaitwa Charlie Mack.

Kwa mujibu wa Documents, Mack ana rekodi ya Makosa ya Jinai... na sheria hairuhusu mtu aliye kwenye kipindi cha muda wa Uangalizi (Probation) kujihusisha na mtu mwenye aina hiyo ya makosa.

Kwa nyakati nyingine mapema jana zilitoka taarifa za Shirika la Ujasusi nchini Marekani (FBI) kuanzisha Uchunguzi dhidi ya mienendo ya Jaji Genece Brinkley.

No comments

Theme images by lobaaaato. Powered by Blogger.