Jike Shupa atolewa vyombo usiku wa manane
Na: Omary Ramsey

Muuza nyago aliyeinogesha video ya mwanamuziki Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’, Zena Abdalah ‘Jike Shupa’ yamemkuta.

Wiki iliyopita Jike Shupa alitolewa vyombo vyake nje kwenye nyumba aliyopanga maeneo ya Mwanyamala, Kwa-Manjunju jijini Dar, kisa kikidaiwa kuwa ni picha chafu anazotupia kwenye mitandao ya kijamii (Instagram). 

Kwa mujibu wa chanzo cha karibu na Jike Shupa, kilidai kuwa, nyumba aliyopanga Jike Shupa inamilikiwa na watu walioshika Dini ya Kiislam.

KISA PICHA ZA UTUPU

Chanzo hicho kiIidai kuwa, Jike Shupa ana tabia ya kutupia picha na video za utupu mitandaoni, jambo ambalo watu anaokaa nao hawalipendi na hata wapangaji wenzake hawataki mtu anayekwenda kinyume na maadili. 

Habari zinazidi kudai kuwa, juzkati Jike Shupa alitupia video kwenye ukurasa wake wa Mtandao Kijamii wa Instagram, ikionesha wanawake wakicheza wakiwa utupu, jambo ambalo liliwakera mno watoto wa mwenye nyumba anayoishi. “Yaani ile nyumba anayoishi Jike Shupa ni ya watu walioshika dini sana, hawapendi kuona mtu anakiuka maadili, hata wapangaji waliowapangisha,” kilidai chanzo hicho.

KUMBE ALISHAONYWA

Chanzo hicho kilizidi kubainisha kuwa, baada ya watoto hao kuona picha hizo walikereka kwa sababu mara kadhaa walishamuonya Jike Shupa kuwa hawapendi kupangisha mtu mwenye tabia kama hizo hivyo walipandwa na hasira na kumuomba aondoke, akatafute sehemu nyingine Chanzo hicho kilizidi kutiririka kuwa, baada ya watoto wa mwenye nyumba hiyo kutoa amri hiyo, Jike Shupa alianzisha timbwili akiwavimbia hivyo kuzidi kuwapandisha hasira na kuanza kurusha vitu vyake nje usiku wa manane. 

“Jike Shupa alikuwa akibishana nao huku wakirushiana maneno makali, jambo ambalo liliwakera watoto wa mwenye nyumba na kuamua kumtolea vyombo nje,” kilizidi kumwaga ubuyu chanzo hicho.

HUYU HAPA JIKE SHUPA

Kwenye mahojiano yake na Ijumaa, Alipoulizwa kuhusu ishu yake hiyo alikiri na kusema kuwa, mtu anapopanga nyumba na kumlipa mwenye nyumba fedha zake za pango, hapaswi kufuatiliwa fuatiliwa. “Yaani wale watu walinizingua sana, mtu nimepangisha na fedha nimetoa, nini shida, nisitangaze shoo yangu? Sasa mimi nitakula wapi? Au fedha ya kodi nitapata wapi? Wala hawajaniumiza kabisa na nimeshapata nyumba nyingine,” alisema Jike Shupa.

Imeandikwa na Omary Ramsey
Chanzo: Ijumaa Wikienda

No comments

Theme images by lobaaaato. Powered by Blogger.