Kanye West akumbusha deni kwa Jay Z

Image result for jayz kanye west


Rapa Kanye West, ameanza kukumbushia deni lake la dola milioni 3.5 kutoka kwa rafiki yake, Jay Z, kutokana na kazi zake zilizofanywa kwenye Kampuni ya Tidal.

Kampuni hiyo inayomilikiwa na Jay Z, ilikuwa inasimamia kazi za muziki za rapa huyo, lakini baada ya kumaliza mkataba wao Kanye West hakulipwa fedha zake na kusababisha wawili hao kuingia kwenye bifu kubwa.

Kanye West ameamua kulifufua bifu hilo baada ya kuanza kudai tena fedha zake alipofanya mahojiano mwishoni mwa wiki iliyopita.

“Jay Z alinipigia simu na kuniuliza kwanini simpigii simu? Nikamwambia yeye ni kama muuaji hivyo siwezi kumpigia bila jambo la msingi, kikubwa ni kuzungumza juu ya fedha zangu, lakini vinginevyo siwezi,” alisema Kanye West. 

Msanii huyo alikuwa miongoni mwa wasanii waliopandisha jina la kampuni hiyo mwaka 2015.

No comments

Theme images by lobaaaato. Powered by Blogger.