Kevin Hart bila kutarajia, akatisha

Kevin Hart bila kutarajia, akatisha Interview ya redio, ni baada ya kuona mke wake amefikia hatua ya mwisho ya kujifungua!

Mchekeshaji huyo wa Marekani aliamua kukatisha interview hiyo ambayo alikuwa akiifanya kwa njia ya simu na kituo cha redio cha Power 95.3 usiku huu ambapo ni majira ya asubuhi kwa Marekani.

Baada ya mke wake kuanza kulia uchungu, meneja wa Kevin aliwaambia hewani kuwa, Eniko anakwenda kujifungua, kisha alikata simu na pamoja wakamkimbiza Eniko hospitali.

Huyu atakuwa mtoto wa kwanza kwa #Eniko na #KevinHart.

No comments

Theme images by lobaaaato. Powered by Blogger.