Kim Kardashian Ataja jinsia ya mtoto wake ajaye

Kim Kardashian ameamua kuweka wazi jinsia ya mtoto wake ambaye anatarajiwa kuzaliwa mapema mwakani.


Akiongea katika kipindi cha The Ellen DeGeneres Show, mrembo huyo amethibitisha kuwa mtoto wake huyo ambaye walipandikiza mbegu kwa mama mwengine atakuwa wa kike.

“Binti yangu anadhani yeye ni muelewa. Tulikuwa na baby shower mwishoni mwa mwa wiki, na nimejifunza, ‘Unajua, ninahitaji baby shower kwa sababu nahitaji [North] kujisikia kwamba kuna kitu kinakuja kwa ajili yake na kumsikiliza,” amesema Kim.

“Kwa hiyo, watu walileta midoli na zawadi na [North] alifungulia siku ya pili. Alisema, Mom, dada hayupo hapa, nafikiria nahitaji hii midoli yote katika chumba changu nicheze nayo na hakikisha yote inakuwa sawa kwa ajili ya mtoto,” ameongeza.
 
Huyo atakuwa ni mtoto wa tatu katika familia ya Kim na mumewe Kanye West, lakini atakuwa ni mtoto w pili wa kike baada ya dada yake North mwenye miaka minne.

No comments

Theme images by lobaaaato. Powered by Blogger.