Kimenuka!! Lil Kim amwita Nicki Minaj ‘Nyoka’
Na: Omary Ramsey

Bifu kati ya rapa Kimberly Jones ‘Lil Kim’ na Nicki Minaj linazidi kupamba moto baada ya mwishoni mwa wiki iliyopita Lil Kim kumwita mpinzani wake ni nyoka.

Ni muda sasa tangu Lil Kim aweke wazi kuwa yeye ni mkongwe wa muziki huo dhidi ya Nicki Minaj na anafanya vizuri kwa kuwa anaiba ‘style’ zake nyingi za uchezaji.

Kwenye mahojiano yake na Ebro In The Morning, Kim alisema, “Kuna rapa wengine hawajielewi, nashangaa kuona mtu unatumia baadhi ya aina zangu za uchezaji jukwaani ili kujitafutia umaarufu, basi kama ni hivyo nipewe heshima yangu.

“Naweza kusema wanawake wa aina hiyo wamekuja kwenye muziki wakibahatisha, kwa yule ambaye ananifuatisha kwangu namwita nyoka,” alisema Lil Kim.

TAZAMA MAHOJIANO YOTE HAPA CHINI

No comments

Theme images by lobaaaato. Powered by Blogger.