KWA HILI... ROMY JONS KAMPIGA BAO DIAMOND PLATNUMZ

Romy Jons au RJ ni moja ya watu wanaounda kampuni ya WCB. Licha ya kuwa Vice President na DJ wa Diamond Platnumz, Romy ni ndugu wa damu kabisa kwa Mwimbaji staa huyo wa Afrika Mashariki.

Miongoni mwa mastaa wa Lebo hiyo, Romy pekee ndiye amekuwa akiweka chini ya kapeti sana ishu zake za mahusiano!! Sasa, utaamini ukisikia taarifa za Romy Jons kutaka kufunga ndoa? Basi acha nikupe Infoz.

Akipiga stori na mtandao wa #Mpasho wa Kenya, Romy alifunguka Exclusive kuwa atafunga ndoa mwezi December mwaka huu.
"I KEEP MY LIFE PRIVATE, BUT I AM GETTING MARRIED IN DECEMBER. I’M NOT GOING TO TELL YOU TO WHOM IT IS, BUT I THINK I’M FINALLY SETTLING DOWN NOW."- alifunguka RomyJons japo aligoma kutuambia ni nani atamuoa.

Kinyume na matarajio ya wengi, Romy Jons atakuwa amempiga bao kaka yake, Diamond Platnumz ambaye bado hajafikia hatua hiyo licha ya kuwa na Watoto Watatu... Wawili (Tiffah & Nillan) akizaa na Zari huku mmoja (Prince Abdul) akimpata kwa mrembo Hamisa Mobetto.


Credit : @info_hd

No comments

Theme images by lobaaaato. Powered by Blogger.