Lavalava Afunguka Kulelewa

Msanii wa muziki wa Bongo Flava kutoka label ya WCB, Lavalava amefunguka ishu ya kuishi katika nyumba ya mwanamke ambaye alimchukulia kama mpenzi wake wakati haikuwa hivyo.


Hitmaker huyo wa ngoma ‘Tuachane’ amesema baada ya kuisha pamoja alikuja kugundua nyumba wanayoishi na mwanamke huyo kapangiwa na mpenzi wake.

“Mwezi mmoja kabla sijaachia Tuachane nilikuwa na mpenzi wangu ambaye tulikuwa tumepanga mipango mingi sana kwamba kuna siku nitafika, nitakuwa hivi na kufanikiwa na kuweza kukuhudumia akawa ananiitikia, fresh kumbe hata pale alipokuwa anakaa kulikuwa kuna mwana kampangia” amesema.

“Mimi nakaa humo humo najiachia, mchizi akarudi hiyo siku nilikuwa kama nihisi kufa kufa hivi, akaniambia bwana nimerudi hapa kwangu” Lalava ameiambia Radio Free Africa.
Ameendelea kwa kueleza kuwa baada ya hilo kutokea waliongea na kujitetea kwa kutoa maelezo ambayo yatakuwa sawa kwa pande zote na kilichofuata ni kwenda kutoa ngoma ‘Tuachane’.

No comments

Theme images by lobaaaato. Powered by Blogger.