Layvin Kurzawa Aweka Record beki wa kwanza kufunga ‘hat-trick’ UEFA

Mchezaji wa klabu ya Paris St-Germain, Layvin Kurzawa amekuwa beki wa kwanza kufunga mabao matatu katika mchezo mmoja “hat-trick” katika michuano ya klabu bingwa barani Ulaya baada ya kufanya hivyo hapo jana dhidi ya Anderlecht na kuisaidia timu yake kufuzu hatua ya 16 bora.
http://a.espncdn.com/combiner/i/?img=/photo/2016/0821/r117467_1296x729_16-9.jpg&w=738&site=espnfc
Mchezaji wa klabu ya Paris St-Germain, Layvin Kurzawa
Kurzawa ambaye ni beki wa kushoto wa klabu ya PSG na timu ya taifa ya Ufaransa amefikisha jumla ya mabao 17 katika mchezo wa soka na hivyo kuweka rekodi ya dunia kuwa na mabao mengi zaidi kuliko beki yoyote.

Katika mchezo huo PSG iliibuka na ushindi wa jumla ya mabao 5-0 huku mshambuliaji wa timu ya taifa ya Brazili, Neymar na Marco Verratti wakiifungia bao mojamoja na kuiwezesha kuingia hatua ya mtoano wakati Bayern Munich wakifanikiwa kutinga hatua hiyo baada ya kuifunga Celtic mabao 2-1.
PSG pia imeweka rekodi ya kuwa na mabao mengi zaidi hatua ya makundi baada ya kuwa na magoli 17 dhidi ya 16 ya Manchester United iliyoweka 998-99.

No comments

Theme images by lobaaaato. Powered by Blogger.