Mbwana Samatta kufanyiwa upasuaji

Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania anayecheza soka la kulipwa nchini Ubelgiji katika club ya KRC Genk,  Mbwana Samatta atakaa nje ya uwanja mpaka msimu wa baridi kutokana na majeraha ya goti aliyoyapata siku ya Jumamosi ya November 4 2017 katika uwanja wao wa Luminus Arena.

Siku ya jana Samatta alipost picha hii na kuonyesha kusikitika kutokana na report hiyo.
Mshambuliaji huyo machachari alikuwa kwenye kikosi cha timu yake katika mchezo wa Ligi Kuu Ubelgiji dhidi ya Lokeren mchezo ambao ulimalizika kwa sare tasa (0-0)
Hata hivyo nahodha huyo wa Taifa Stars hakumaliza dakika 90 za mchezo kutokana na jeraha hilo na nafasi yake kuchukuliwa na Mgiriki, Ubelgiji.Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na klabu hiyo baada ya Samatta kufanyiwa vipimo, imegundulika kuwa jeraha lake hilo litamuweka nje ya uwanja hadi kipindi cha majira ya baridi.

No comments

Theme images by lobaaaato. Powered by Blogger.