MEEK MILL AANZA KUNUSA HARUFU YA NJE

Huenda rapa Meek Mill asimalize kifungo chake cha miaka miwili jela.

Mwanaharakati wa Marekani Alfred Charles Sharpton maarufu kama 'Al Sharpton' amepanga kumtoa jela rapa Meek Mill.

Akizungumza kwa uzoefu alionao baada ya kuwahi kumtoa jela hayati Tupac Shakur, Al Sharpton alisema Jumatatu hii itakuwa ndio mwanzo wa mchakato huo ambapo amepanga kuzungumza na Mamlaka ya gereza la Pennsylvania na kuhakikisha pia Jaji Genece Brinkley anaondolewa kwenye kesi hiyo.

Leo Jumatatu, #Sharpton atamtembelea rapa Meek Mill katika gereza la Chester State mjini Philadelphia.

Upande mwingine, Unaambiwa Meek Mill aliwekwa jela ya peke yake (Sonitary Confinement) kutokana na hadhi yake, lakini kwa sasa ameomba achanganywe na wafungwa wenzake.

No comments

Theme images by lobaaaato. Powered by Blogger.