MEEK MILL MATATANI.. HUENDA AKAFUNGWA MIAKA MIWILI

Rapa Meek Mill ameingia kwenye matatizo makubwa ya kisheria.. matatizo ambayo huenda yakapelekea kufungwa Jela kwa miaka Miwili.

Rapa huyo ambaye jina lake kamili ni Robert Rihmeek Williams, atahudhuria Mahakamani Jumatatu ijayo kwa makosa ya uvunjaji wa Masharti ya muda wa Uangalizi (Probation) aliyowekewa kwenye kesi yake ya kukutwa na Madawa ya kulevya pamoja na silaha za moto ya mwaka 2008.

Ukiwa kwenye muda wa uangalizi (Probation), hauruhusiwi kufanya kosa lolote la uvanjaji wa sheria... Hivyo Jaji wa kesi hiyo ameweka wazi makosa mawili aliyofanya rapa Meek Mill.

Kwanza: Kukamatwa baada kupigana katika uwanja wa ndege wa St. Louis mwezi March.

Pili: Kukamatwa kwa kosa la Uendeshaji Mbovu wa chombo cha moto, mwezi August mwaka huu.

Tayari #MeekMill amewahi kuwekwa kifungo cha ndani (House Arrest) baada ya kuvunja sharti hilo la muda Uangalizi, ni baada ya kusafiri bila ruhusa ya Mahakama.. ila kwa Makosa haya mawili ya sasa... MEEK MILL yupo kwenye hati hati ya KUFUNGWA JELA MIAKA MIWILI.

No comments

Theme images by lobaaaato. Powered by Blogger.