MIMI MARS AENDELEA KUSHIKA MAWILI

Image result for Mimi MarsMsanii kutoka Mdee Music "Mimi Mars" amesema kuwa kwasasa hafikirii kuacha kutangaza kwasababu ya kufanya muziki mpaka pale kimoja kitakapozidi kitu kingine.

Mimi Mars amekiambia kipindi cha TOP HITZ kinachorushwa kupitia Dream Fm Mbeya na Mtangazaji Ergon Elly kuwa haoni kama kunaulazima wakuacha kitu kimoja kwasasa kwani kutangaza na kufanya muziki vyote kwa wakati mmoja anavimudu.

Lakini msanii huyo ambaye ametambulisha pini lake jipya, 'SITAMANI', amewataka wasanii wenzake wa kike kushirikiana kama ambavyo wasanii wakiume wa bongo wanavyofanya ili muziki wao ufanikiwe kama wasanii wa kiume wa Bongo Fleva.

No comments

Theme images by lobaaaato. Powered by Blogger.