Mkuu Wa Mkoa Mh. Makonda asisitiza kupiga muziki mwisho saa 6 usikuMkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametoa onyo zito kwa watu ambao wamekuwa wanapiga muziki katika maeneo ya wazi na kusumbua wengine kuanzia saa sita usiku na kuendelea.Kiongozi huyo amesema utaratibu upo ambao unaonyesha kuwa kupiga muziki katika maeneo ya wazi ni mwisho saa sita usiku na sio vinginevyo na endapo mtu atahitaji kufanya hivyo ni bora akapige katika klabu za usiku ambapo ndio wameruhusiwa kufanya hivyo.

Akiongea katika kipindi cha Joto la Asubuhi cha EFM Ijumaa hii, Makonda amesema, “Kuna watu wanasauti ya kusema sana lakini wengi ambao hawana sauti ya kusema ndio wanaumia. Ukitoka hapa Makumbusho ukienda mbele kidogo kuna bar walikuwa wanapiga, ile bar muziki uliokuwa ukipigwa ikifika saa sita utafikiri hawasikilizani pale, wanaongeza sauti kiasi kwamba hospital ya Kairuki hapa wagonjwa wanalia.”

“Nilishasema zipo taratibu, ukitaka kupiga muziki kuanzia saa sita na kuendelea nenda kwenye klabu. Mpaka dakika hii ninavyoongea sheria haijabadilika saa sita ni mwisho, na kama askari wangu wapo huko wananisikia kupitia EFM wafahamu. Sitaki kusikia muziki unapigwa kwenye majengo ya watu ya wazi na kusumbua watu wengine,” ameongeza.

No comments

Theme images by lobaaaato. Powered by Blogger.