Nandy: Kolabo na Wizkid itapendeza

Related image


Msanii wa muziki wa Bongo Fleva na mshindi wa tuzo ya Afrima ya Mwanamuziki Bora wa Kike Afrika Mashariki, Faustina Charles 'Nandy', amesema anafikiri kufanya kolabo na nyota wa Nigeria, Wizkid.

Akizungumza hivi karibuni, Nandy alisema tayari amepata mawasiliano na menejimenti ya msanii huyo wa Nigeria na anafikiria kumshirikisha kwenye nyimbo yake kwa siku zijazo.

"Ni jambo ambalo limekuwa kwenye ndoto zangu, nimepata bahati ya kukutana naye Nigeria nilipokwenda kwenye utoaji wa tuzo na tumebadilishana mawasiliano, nataka ndoto yangu itimie kufanya wimbo na Wizkid kwa sababu ni mmoja wa wanamuziki ninaowakubali zaidi," alisema Nandy.

No comments

Theme images by lobaaaato. Powered by Blogger.