"Nasumbuliwa sana kisa wowowo" - ZaiidBila shaka wimbo wa Zaiid 'wowowo' umeanza kushika kasi na kupendwa na watu wengi mpaka kufikia hatua ya usumbufu kuongezeka kwa msanii huyo baada ya mashabiki wengi na marafiki zake kuomba namba wakihitaji mawowowo yaliyomo kwenye wimbo wa 'wowowo'.

"watu wamekuwa wakinisumbua sana katika mitandao ya kijamii na kwenye simu wakiniulizia namba za wale mabinti ambao wamecheza katika wimbo wa wowowo wakiwataka kimapenzi , ila mimi huwa nawaambia kuwa watu hao sina namba zao kwa sababu Riyama Ally yule msanii wa bongo movie ndio aliniunganisha nao" , alisema Zaiid

Zaiid ni moja kati ya wasanii ambao wanafanya vizuri kwa sasa kutokana na staili yake ya uimbaji.

ZAiiD - Wowowo


No comments

Theme images by lobaaaato. Powered by Blogger.