Olympiakos yavunja rekodi ya Barcelona

Klabu ya Barcelona ya nchini Hispania hapo jana usiku imetoka sare ya bila kufungana kwa mara ya kwanza katika hatua ya makundi ya michuano ya klabu bingwa barani Ulaya baada ya kupita zaidi ya miakia mitano.Katika mchezo wa kundi D, Barcelona imetoka sare ya bila kufungana dhidi ya Olympiakos huku wachezaji wake tegemezi, Luis Suarez na Lionel Messi wakishindwa kuona lango la timu pinzani.


Licha ya kuambulia sare ya 0-0 dhidi ya Olympiakos, kikosi cha Barca kinaongoza katika msimamo wa kundi D kwakuwa na pointi 10 ikiizidi Juventus wenye alama 7 baada ya hapo jana nao kutoka sare ya 1-1 na Sporting Lisbon.

 Barca itahitaji kushinda katika michezo miwili iliyosalia dhidi ya Juventus na Sporting ili kujihakikishia nafasi ya kuingia hatua ya 16 bora

No comments

Theme images by lobaaaato. Powered by Blogger.