Rapa B.O.B ameendelea kuwa mtafiti na kuichunguza dunia kiundani.

Baada ya kuja na Theory zake na kutuambia dunia ni tambarare na sio duara!! B.O.B sasa amekuja kuwaletea changamoto watu Historia, ameibuka na kupinga kuwahi kuwepo kwa BIASHARA YA UTUMWA.

Akiutumia ukurasa wake wa Instagram Juzi Jumatano, B.O.B ambaye jina lake kamili ni Bobby Ray Simmons, Jr. alipost video iliyoambatana na maelezo haya,
"They say slavery lasted 400 yrs... America is only 250 yrs old... You ever seen a slave ship ? They can find a billion year old dinosaur bone but can't find any slave ships. #AseerTheDukeofTiers #apparently #SlaveryIsNotInMyDNA #WeBeenHere

B.O.B amekuja kupingana na historia inayosema, biashara ya utumwa ilidumu kwa miaka 400.. wakati taifa la Marekani lina umri wa miaka 250.

Kingine kinacholeta ukakasi kwa Rapa huyo ni kukosekana kwa Ushahidi wa meli za kusafirisha watumwa hao (Slave ships)! Anasema kama waliweza kuthibitisha uwepo wa mnyama (dinosaur) kwa kutuonesha mifupa yake iliyoishi miaka bilioni, kwanini washindwe kutuonesha Meli hizo?

Hivyo, The "Nothnin' On You" rapper B.O.B alihitimisha kwa kusema, Hana damu ya utumwa kama inavyoaminika kuwa watu weusi (Black People) asili yao ni bara la Afrika na waliingia Marekani kupitia biashara ya utumwa.

Anaamini walikuwepo Marekani Miaka nenda, miaka rudi.

Una maoni gani juu ya kauli hii ya B.O.B? Niachie comment yako hapa

No comments

Theme images by lobaaaato. Powered by Blogger.