Rich Mavoko kuhusu ku-date na Gigy Money na Lulu Diva

Msanii wa Bongo Flava kutoka label ya WCB, Rich Mavoko amesema hakuna ukweli wowote kuhusu yeye kutoka kimapenzi na Gigy Money na Lulu Diva.Muimbaji huyo amekiambia kipindi cha The Playlist, Times Fm kuwa hasa ishu ya Gigy Money ni stori za kutengeneza tu hasa pale alipomuimba katika ngoma ya ‘Mpe Habari’ abaymo alifanya na Stereo.

“Sema mimi sijawahi kusema natoka naye labda yeye atangaze kwa kuamua kuongea lakini nafikiri ni vitu ambavyo vimeshapita hata kuviongelea huwa staki” amesema.

Kuhusu Lulu Diva, Mavoko amesema wao ni marafiki tu wa kawaida na hivi karibuni hawajaonana kutoka Lulu alikuwa bize na show zake.

Tena sijaonana naye muda huwezi amini, nimekuja kuonana naye hivi karibuni kwa sababu na yeye alikuwa yupo bize alikuwa na show, ndivyo anavyoweza kulizungumzia.

No comments

Theme images by lobaaaato. Powered by Blogger.