Rick Ross, Fat Joe, T.I wamkingia kifua Meek Mill

Related image


Wasanii mbalimbali wa muziki wa hip hop nchini Marekani, wameungana pamoja na kuonesha sapoti yao kwa mwenzao, Meek Mill, ambaye anaweza kwenda jela miaka miwili hadi minne kwa kukutwa na silaha kinyume na utaratibu pamoja na kujihusishwa na dawa za kulevya.

Wiki iliyopita msanii huyo alifikishwa mahakamani kutokana na kesi hiyo ambayo ilianza mwaka 2009, hivyo kutokana na mashtaka yake kuna uwezekano mkubwa wa kwenda jela.

Rapa Jay Z, Rick Ross, T.I, Fat Joe na wengine wengi wamejitokeza kwa kuonesha sapoti na upendo kwa nyota huyo kutoka Philadelphia.

Jay Z alitumia ukurasa wake wa Instagram na kusema: “Sidhani kama Meek Mill ana kosa lolote, ninaamini tutaendelea kuwa na yeye,” aliandika Jay Z, wakati huo T.I. alisema: “Watu wote wa muziki wa hip hop tupo na wewe, Mungu pia yupo na wewe,” aliandika T.I.

No comments

Theme images by lobaaaato. Powered by Blogger.