RIHANNA AMTAKA DJ BLACK COFFEE WA S.AIlikupita hii? Sasa acha nikusogezee.. Mwanadada Rihanna amtaka DJ Black Coffee wa Afrika Kusini .. azimika na mikono yake, ataka wafanye kitu.

Akipiga stori na Metro FM ya Afrika Kusini, DJ huyo ambaye pia ni Mtayarishaji wa muziki alifunguka Exclusive! kuwa, kambi ya Rihanna ilimtafuta na kumwambia Riri anataka kufanya naye wimbo baada ya kusikia kazi aliyoifanya na Cassie. Hivyo Coffee akawatumia baadhi ya nyimbo, wakachagua mmoja na kumpa mrejesho kuwa Rihanna yupo tayari, na kazi imeanza ya kuupika wimbo huo.
Image result for rihanna & dj coffee

Black Coffee ambaye ni mshindi wa Tuzo ya BET: Best International Act: Africa mwaka 2016, amefunguka pia stori yake ya kuikacha kazi ya Jay-Z kwenye album ya 4:44

Black anasema alikuwa nchini Italia ambapo alipokea simu kutoka Swizz Beatz akimwambia Jay anataka kufanya naye kazi moja kabla hajakamilisha album yake.

Kusikia habari hiyo, Kwa uoga, furaha na kushindwa kujizuia, huwezi amini Black Coffee alishindwa kufanya kazi hiyo.

"Swizz reached out and said Jay is looking for one song before he concludes his album. It freaked me out. I am in Milan, I couldn't sleep. He literally called me: 'I spoke to Jay. Jay wants a song.' I couldn't sleep. Then I didn't work. I couldn't. How do you produce a song for Jay -Z? He kept saying: Ýo, man. I'm waiting'. I think I failed him but subconsciously I think I wanted to. I wasn't ready."- alisema Mtayarishaji/DJ huyo.

Mbali na Cassie, Rihanna na Jay-Z, wakali wengine wa dunia waliomtokea na kuomba Colabo ni Usher Raymond, Akon na Diddy.

No comments

Theme images by lobaaaato. Powered by Blogger.