Rihanna atajwa ku-Host Onyesho la Mavazi la MET GALA 2018.

Baada ya kuwa gumzo kwenye Onyesho la mwaka 2017, Mwimbaji huyo staa kutoka visiwa vya Barbados, atasimama na ku-Host Onyesho hilo la mavazi ambalo huwakutanisha watu maarufu na kuonyesha ujuzi wao kwenye Mavazi.

Met Gala huwa ni maalum kwa kuchangia na kukuza mfuko wa chuo cha Makumbusho ya Sanaa na mavazi mjini New York, (Metropolitan Museum of Art's Costume Institute) ambapo kauli mbiu ya mwaka ujao inasema, "Heavenly Bodies: Fashion and the Catholic Imagination."
-
Rihanna pia atasimama na mastaa wengine wawili, Donatella Versace na Amal Clooney. Onyesho limepangwa kufanyika Mei 7, 2018.

No comments

Theme images by lobaaaato. Powered by Blogger.