Serena Williams kufunga Ndoa Kesho! Umeripoti mtandao wa page Six.

Taarifa kutoka ndani ya familia yake inasema, Serena Williams na mchumba wake, Alexis Ohanian watafunga ndoa kesho Alhamis katika ukumbi wa Contemporary Arts centre mjini New Orleans Marekani.

Wawili hao ambao wamebarikiwa mtoto mmoja, Alexis Olympia Ohanian Jr. wameamua kuifanya kwa SIRI harusi hiyo.

Tunaambiwa wageni wamepigwa marufuku kusambaza picha mitandaoni, na #SerenaWilliams tayari ameingia mkataba na Mtandao wa 'Vogue' ambao utahusika kwa picha Exclusive za harusi hiyo.

No comments

Theme images by lobaaaato. Powered by Blogger.