SNOOP AENDELEA KUMVUTA SHARUBU DONALD TRUMP

Rapa Snoop Dogg alianza kwa kumnyooshea bastola kichwani Rais Donald Trump!!! Na sasa amehamia kwenye kuumaliza mwili wake kabisa! Huku akidokeza kilichoonekana ni ujio wa album yake mpya.

Siku ya Jumanne, Rapa huyo aliutumia ukurasa wake pendwa wa Instagram na ku-post picha hii ambayo inaonekana ni Cover ya album yake mpya! "Make America Crip Again" (Kuitengeneza Marekani isiyojiweza tena) Huku ikimuonesha Trump akiwa amefariki.

Cover hii pia ni mfanano wa album ya rapa Ice Cube "Death Certificate" ya mwaka 1991.

Dunia nzima inafahamu ni kiasi gani #SnoopDogg anamchukia na hafurahishwi na utawala wa Rais huyo wa sasa wa Marekani.

No comments

Theme images by lobaaaato. Powered by Blogger.