Steve Nyerere amuonya Afande Sele

Msanii wa Filamu Bongo, Steven Nyerere amefunguka kufuatia kauli ya msanii Afande Sele aliyoitoa hivi karibuni kuhusu Marehemu Steven Kanumba mara baada ya Elizabeth Michael ‘Lulu’ kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili jela kwa kosa la kumuua bila kukusudia msanii huyo.Hivi karibu baada ya hukumu hiyo Afande Sele aliibuka na kuandika ujumbe wa kumshtumu Kanumba kwa kitendo cha kutembea na Lulu wakati akiwa bado mdogo, huku akieleza hakushiriki kivyovyote katika msiba wa msanii huyo ingawa alikuwepo Dar kwani hakutaka kuvaa joho la unafki.

Sasa Steve Nyerere katika mahojiano na E-Newz ya EATV amesema muda mwingine wasanii wawe na busara kwa kile wanachokiongea kwani Watanzania wanawaangalia na kuwapima kwa kauli zao.
“Usikurupuke tu, nakumshutumu Marehemu, yaliyopita sisi mbele tungange yajayo. Tunapotaka kufanya kitu jiangalie kwanza, halafu sema mimi ninayeongea jamii nje ninayoingoza naifundisha nini, kuna vitu vingine vinaongelewa hapa ni uchochezi tu, ni uchochezi wa kuua sanaa, mbaya sana” amesema.

Ameongeza kuwa kwa sasa kila mmoja anataka kufukua jambo hilo na wengine wanataka kupata umaarufu kupitia hilo. “Wengine mastaa wa zamani wanataka kujifanya wanalijua kuliongelea hili ili nao wachipukie hapo hapo” amesisitiza.

No comments

Theme images by lobaaaato. Powered by Blogger.