Unawakumbuka Spice Girls?


Unawakumbuka Spice Girls? Sasa baada ya kupotea kwa takribani miaka Mitano... wamepanga kurejea kwenye muziki.. ila mke wa David Beckham kajitoa!

Taarifa kutoka ndani ya kundi hilo zinasema Victoria Beckham, maarufu kama 'Posh Spice', amejitoa na hatakuwepo kwenye Ujio mpya wa kundi hilo ambao umepangwa kufanyika mwaka 2018 ukiambatana na album mpya.

Kundi la #SpiceGirls ni muunganiko wa Wasichana watano wa Kiingereza: Melanie Brown, Melanie Chisholm, Emma Bunton, Geri Halliwel na Victoria Beckham.

Kundi hilo liliundwa mwaka 1994, na walitamba na nyimbo zao kama: Viva Forever, Mama, Wannabe, Who Do You Think You Are na zingine kibao. Huku wakifanikiwa kuachia jumla ya album 3.

Wakali hao wa Pop pia waliwahi kuitikisa dunia kwa Album yao ya Kwanza "SPICE" kuuza zaidi ya nakala Milioni 31 dunia nzima na kuweka rekodi ya album bora kuwahi kuuzwa na kundi la kike la muziki.

No comments

Theme images by lobaaaato. Powered by Blogger.