Wilder Amtamani Anthony JoshuaBondia wa uzito wa juu nchini Marekani, Deontay Wilder amesisitiza kuwa yupo tayari kupigana na bingwa wa dunia wa uzito wa juu Muingereza, Anthony Joshua na kamwe hawezi kuipoteza nafasi hiyo hadhimu.


Bondia wa uzito wa juu nchini Marekani, Deontay Wilder 

Chombo cha habari cha Sky Sports kupitia mahojiano yake na meneja wa Joshua, amesema wanatarajia kuanza kufanya mazungumzo na bondia Wilder wiki hii ili kufikia muafaka wa pambano hilo.

Wakati bingwa huyo wa WCB, Wilder amethibitisha kuanza kufanyika kwa mazungumzo hayo lakini amemtaka mfalme wa IBF na WBA, Anthony Joshua kutokufanya maamuzi mengine kabla ya kikao chao kilichopendekezwa.

“Tupo katika mazungumzo na tutakapo fika muafaka tutaweka wazi.” Wilder amekiambia chombo cha habari cha Sky Sports.
“Kila ninachozungumza ni jukumu la Eddie Hearn na sio Joshua. Ujumbe wangu kwa Joshua nipo tayari kwa mpambano.”
Wilder mecheza mapigano 39 bila kupigwa hata moja huku mwishoni mwa wiki iliyopita alifanikiwa kutetea mkanda wake wa  WBC dhidi ya Bermane Stiverne.

No comments

Theme images by lobaaaato. Powered by Blogger.