YCEE KIMENUKA!!! ATAKA KUIKACHA SONY MUSIC

Image result for YCEE
Mwimbaji kutoka pande za +234 Nigeria, YCEE amefumua bomu kuhusu uhusiano wake na lebo ya SONY MUSIC ENTERTAINMENT, adai wanata kumuharibia maisha yake ya muziki.

YCEE ambaye alisainiwa na lebo hiyo kubwa duniani October 21 mwaka 2016, ameibuka kupitia ukurasa wake wa Twitter na kuwashukia SONY akidai walimfata na kumuahidi kumsaidia kukua kimuziki lakini lengo lao ni kumuharibia tu! ILA tayari amepata mpango mpya!

Akiendelea kujilipua, staa huyo wa 'Omo Alhaj', aliendela kutupa mabomu na kuwataadharisha Wasanii wengine kuwa makini,
"..'ll speak as much as I can to prevent others from being a VICTIM. Too many artistes stay silent and make others suffer the same cause."- aliandika #YCEE kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Huyu anakuwa msanii mwingine kutoka Nigeria kuilaumu lebo hiyo, alianza Davido ambaye alijitoa kabisa. Wengine pia kutokea afrika ambao waliikacha ni REDSAN; KEKO na DBanj.

SONY MUSIC ENTERTAINMENT ndio lebo ambayo pia imemsaini staa wa Bongo Fleva, Ali Kiba 

No comments

Theme images by lobaaaato. Powered by Blogger.