Zlatan Ibrahimovic Ana kwa ana Manchester City

Meneja wa klabu ya Manchester United, Jose Mourinho amekiambia chombo cha habari cha Sky Sports kuwa kabla mwaka huu haujamalizika basi mshambuliaji wa timu hiyo, Zlatan Ibrahimovic atakuwa amesharejea uwanjani.


Mshambuliaji huyo aliyekuwa akiuguza majeraha yake ya goti huenda akawa tayari kuikabili Manchester City mwezi ujao.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari cha gazeti la The Sun kimeripoti kuwa wachezaji wote wawili Zlatan na Paul Pogba watakuwepo katika mchezo wa wikiendi hii dhidi ya Newcastle.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35, ameanza kurejea katika mazoezi Carrington mwezi Oktoba huku Mourinho akisema kuwa Ibrahimovic atarejea mwishoni mwa mwaka 2017.

“Yeye ni Simba, mpambanaji na anahasira kuona yupo nje kwa muda mrefu ndiyo sababu kubwa yakurejea kwake,” amesema Mourinho.

Mwezi uliyopita daktari anaye mhudumia Ibrahimovic , Freddie Fu alionya mchezaji huyo asichezeshwe katika mchezo dhidi ya Anderlecht wa michuano ya Europa League mwezi Aprili.

Ibrahimovic ndiye mchezaji aliyefunga mabao mengi zaidi msimu uliyopita ndani ya United baada ya kutupia magoli 28, amesaini mkataba wa mwaka mmoja mwezi Agosti.

No comments

Theme images by lobaaaato. Powered by Blogger.