Babu Seya ‘OUT’, Mastaa wazungumza

Image result for Babu Seya


Na: Omary Ramsey

Baada ya kifungo cha miaka 13 jela,  ndoto ya wanamuziki Nguza Viking ‘Babu Seya’ na mwanawe, Johnson Nguza ‘Papi Kocha’ kurudi uraiani imetimia mara baada ya Rais Dk. John Magufuli, kutangaza msamaha kwao katika maadhimisho ya 56 ya Uhuru wa Tanganyika yaliyofanyika juzi mkoani Dodoma.

Juni 25 mwaka 2004, mastaa hao wa singo ya Tutoke Wote, walitiwa hatiani kwa kosa la kubaka na kunajisi watoto ambapo rufaa yao waliyoikata mwaka 2010 ilizaa matunda na hukumu ikatolewa, ambapo watoto wawili wa Babu Seya Mbangu na Francis Nguza waliachiwa huru huku yeye na Papi Kocha wakiendelea kutumikia kifungo katika Gereza la Ukonga, Dar es Salaam.

Si mashabiki tu bali na mastaa kadhaa wa Bongo Fleva nao wameonyesha kuguswa na msamaha wa Rais kwa wanamuziki hao na kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii wameweza kuonyesha hisia zao.

Diamond Platnumz: More than a Presdent, Tanzania is so lucky to have you.

Wema Sepetu: Shoutout to Serikali ya Awamu ya 5, asante Rais wangu, karibuni uraiani wapendwa, we sure missed you, to my brother Papi, nakumbuka barua zako ulizokuwa unaandika kuomba hata niweze kuongea na viongozi ili muwe considered kuhusu uhuru wenu, u got it now kaka akee, welcomback.

Ali Kiba: Najivunia kuwa Mtanzania.

Joti: Hakika Mungu huwa hasinzii, Mungu ni hakimu wa kweli, nasema usikate tamaa kama bado unapumua, karibu Papi Kocha kitaa tupige kazi.

No comments

Theme images by lobaaaato. Powered by Blogger.