Ed Sheeran Alivyoiweza Hesabu Ngumu Ya 2017


Miongoni mwa Albamu zilizouza na bado zikaendelea kufanya vizuri kwenye charts tofauti ipo 'Divide', Albamu iliyokuja na ngoma kadhaa Kali ikiwemo hitsong "Shape Of You".
 Baada ya mafanikio ya 'Shape Of You' , Ed Sheeran anaonekana kuendelea kujikusanyia nafasi kubwa ya kumfanya aitwe mfalme wa mitandao inayotoa huduma ya kuuza na kusikiliza nyimbo.


Kwenye mtandao wa iTunes ngoma 100 zinazouza zaidi zinaongozwa na Perfect ya Ed Sheeran.


Perfect Symphony imefanywa na Ed Sheeran & Andrea Bocelli ndio ngoma inayofanya vizuri kwenye mtandao wa iTunes ikifuatiwa na Perfect (Original) ambayo ipo nafasi ya pili kwenye list ya ngoma 100 zinazotrend iTunes.

 
Ngoma nyingine inayosikilizwa zaidi kwa sasa ni 'River' ya Eminem ambayo ameshirikishwa Ed Sheeran, River ni ngoma inayosikilizwa zaidi Kwenye mtandao wa Spotify  ambao mwezi Novemba ulitoa orodha ya ngoma Na wanamuziki waliosikilizwa zaidi na Of course Ed Sheeran alitajwa kuwa wa kwanza.


Shazzam kwenye ngoma zake 100 zinazotafutwa zaidi ni Perfect ya Ed Sheeran inayoimiliki nafasi ya kwanza

Billboard Top 100 namba moja inamilikiwa na Ed Sheeran takribani wiki tatu

No comments

Theme images by lobaaaato. Powered by Blogger.